𝐔𝐉𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀 “𝐒𝐄𝐑𝐄𝐍𝐆𝐄𝐓𝐈 𝐍𝐀𝐓𝐈𝐎𝐍𝐀𝐋 𝐏𝐀𝐑𝐊 𝐆𝐎𝐋𝐅 𝐂𝐎𝐔𝐑𝐒𝐄” 𝐖𝐀𝐅𝐈𝐊𝐈𝐀 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝟒𝟐

 

𝐔𝐉𝐄𝐍𝐙𝐈 𝐖𝐀 “𝐒𝐄𝐑𝐄𝐍𝐆𝐄𝐓𝐈 𝐍𝐀𝐓𝐈𝐎𝐍𝐀𝐋 𝐏𝐀𝐑𝐊 𝐆𝐎𝐋𝐅 𝐂𝐎𝐔𝐑𝐒𝐄” 𝐖𝐀𝐅𝐈𝐊𝐈𝐀 𝐀𝐒𝐈𝐋𝐈𝐌𝐈𝐀 𝟒𝟐



Ujenzi wa mradi wa kimkakati wa uwanja wa gofu Hifadhi ya Taifa Serengeti “Serengeti National Park Golf Course” uliobuniwa na Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania chini ya Mwenyekiti wake Jenerali (Mstaafu) George Waitara unaojengwa katika eneo la Fort Ikoma, nje kidogo ya Hifadhi ya Taifa Serengeti umefikia asilimia 42.


Utekelezaji huo unajumuisha ujenzi wa “Tee and Green” kwa mashimo kumi na nane; mashimo tisa ya kwanza (front- nine/inbound holes),  mashimo tisa ya nyuma (back - nine/outbound holes), uchimbaji wa visima virefu viwili vyenye uwezo wa kutoa maji kiasi cha lita elfu kumi kwa saa kwa kila moja, uchimbaji na ujenzi wa mabwawa ya maji mawili yenye ujazo wa takribani lita millioni 22 kila moja, ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 5.2 kuzunguka uwanja mzima, ujenzi wa “power house” na ufungaji wa pampu za maji pamoja na “ solar panels ” kwenye visima viwili vilivyochimbwa.


Msimamizi wa mradi huu, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Mhandisi Mshauri, Dkt. Richard Matolo alieleza upekee wa uwanja huu kuwa ni pamoja na kuongezwa urefu kwa kila shimo (unaojumuisha “Tee Fairway” na “Green” ), hivyo kuufanya uwanja huu kuwa moja ya viwanja virefu duniani, kupindishwa kwa baadhi ya mashimo “dog legging” na uwepo wa miti kwenye baadhi ya mashimo na hivyo kuwa changamoto kubwa kwa mchezaji.


“Ni uwanja wa kipekee ukilinganisha na viwanja vingine vya gofu duniani. Upekee wa uwanja huu siyo tu kwa sababu unajengwa kwenye eneo la hifadhi maarufu duniani ya Serengeti, bali pia unatokana na sifa za makusudi zilizoongezwa kwenye usanifu wake. Ni watu wachache sana ambao ni wachezaji bingwa wa gofu watakaoweza kucheza na kumaliza ndani ya vigezo vinavyotambulika kimataifa.” aliema Dkt. Matolo. 


Wakizungumza mara baada ya kucheza kwa mara ya kwanza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini TANAPA Jenerali Mstaafu George Waitara katika uwanja huo. Mhe. Balozi Charles Sanga, Mhe. Balozi Job Masima na Mhe. Dkt. Edmund Mndolwa walifurahi kucheza katika uwanja huo kwa mara ya kwanza.




Vilevile, Mhe. Dkt. Mndolwa alieleza kuwa “Huu ndio umekuwa mchezo wa kwanza wa kihistoria, nawapongeza sana Menejimenti ya TANAPA kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kujenga utalii wa michezo na diplomasia ya gofu.


Naye, Balozi Mhe. Job Masima alisema “Uwanja huu ni Game Changer, hakuna uwanja utaenda duniani ukakuta ni mkubwa kiasi hiki wenye mandari nzuri na wanyama.


Aidha, Balozi Charles Sanga alieleza kuwa “Ile ndoto yetu ya kuwa na uwanja wa kisasa wa Gofu Serengeti tunaona inaenda kutimia na maendeleo ya ujenzi wa uwanja huu ni mazuri sana”.


Mradi huu unatoekelezwa katika eneo lenye ukubwa wa ekari 450 utagharimu kiasi cha shilingi bilioni tisa na nusu unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025.



Comments

Popular posts from this blog

General Information: Kilimanjaro Climbing, Safari In Tanzania, Zanzibar Island, Tanzania Wild Camps and Zara Charity

Tanzania Named Top African Safari Destination by Global Customer Analysis

Danish Lady Breaks a Record After Climbing Mount Kilimanjaro for 5hrs and 52 minutes with Zara Tours