BODI YA UTALII (TTB) NA TURKISH AIRLINES KUSHIRIKIANA KUIMARISHA UTALII TANZANIA
BODI YA UTALII (TTB) NA TURKISH AIRLINES KUSHIRIKIANA KUIMARISHA UTALII TANZANIA Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii TTB, Bw. Ephraim Mafuru kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Turkish Airlines Bw. Abdulkadir Karaman wakibadilishana nyaraka za makubaliano mara baada ya kutia saini makubaliano ya ushirikiano kati yao kutangaza utalii wa Tanzania Katikati ni Mkurugenzi wa Utalii wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Dr. Thereza Mugobi Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii TTB, Bw. Ephraim Mafuru kushoto na Mkurugenzi Mtendaji wa Turkish Airlines Bw. Abdulkadir Karaman wakionesha nyaraka za mikataba hiyo zenye makubaliano mara baada ya kutia saini na kuanzisha ushirikiano kati yao kutangaza utalii wa Tanzania, ………………… Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeanzisha ushirikiano wa kimkakati na Shirika la Ndege la Uturuki (Turkish Airlines) kwa mkataba wa miaka mitatu, ukiwalenga kukuza utalii wa Tanzania katika masoko ya kimataifa. Ushirikiano huo unalenga kutumia mtandao...