ZARA TANZANIA ADVENTURES YAZINDUA “TWENZETU KILELENI MSIMU WA 5” NA “TWENZETU SERENGETI”
ZARA TANZANIA ADVENTURES YAZINDUA “TWENZETU KILELENI MSIMU WA 5” NA “TWENZETU SERENGETI”
Dar es Salaam, 10 Septemba 2026 – Zara Tanzania Adventures imezindua rasmi kampeni za “Twenzetu Kileleni – Msimu wa 5” na “Twenzetu Serengeti” katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika National College of Tourism, karibu na IFM City Center, Dar es Salaam.
Kampeni hizo zinalenga kuhamasisha Watanzania, taasisi za Serikali na binafsi,
makampuni, mashirika, vyuo,
vikundi na jamii
kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika
utalii wa ndani, huku wakijivunia na kuthamini vivutio vya kipekee ambavyo Tanzania imebarikiwa navyo.
Kupitia Twenzetu Kileleni – Msimu wa 5, washiriki watapata fursa ya kupanda Mlima
Kilimanjaro kupitia Njia
ya Marangu na kufika kileleni tarehe 9 Desemba 2026, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 65 ya Uhuru wa Tanganyika. Gharama maalum ya ushiriki ni Shilingi
1,800,000 kwa mtu,
ikijumuisha huduma muhimu
za safari kama malazi,
chakula, usafiri, tozo za Serikali,
huduma za waongoza
mlima, wapagazi, wapishi na vifaa muhimu vya kupandia mlima.
Mbali na safari ya kuelekea kileleni,
washiriki wa Twenzetu
Kileleni pia watapata nafasi ya kupanda
miti kama sehemu ya mchango
wao katika kuhifadhi
mazingira na kuongeza uoto
wa asili. Miche
hiyo itatolewa na Zara Tanzania Charity, taasisi inayotekeleza miradi mbalimbali ya kijamii na
kimazingira kwa lengo la kusaidia jamii na kuchangia maendeleo endelevu nchini
Tanzania.
Hatua hiyo inalenga kuifanya
safari ya Twenzetu
Kileleni kuwa zaidi ya tukio la
kupanda mlima, kwa kuwa washiriki pia wataacha alama
chanya katika mazingira kupitia upandaji wa miti na
kuhamasisha umuhimu wa utunzaji wa mazingira.
Kwa upande mwingine, Twenzetu Serengeti inalenga kuwapa Watanzania nafasi ya
kujionea moja kwa moja utajiri wa wanyamapori na mandhari
ya Tanzania kupitia safari inayojumuisha maeneo maarufu ya Tarangire,
Serengeti na Ngorongoro.
Gharama ya safari ni Shilingi 1,200,000 kwa mtu,
ikiwa ni bei maalum kwa kundi la
watu wasiopungua saba.
Safari hiyo inajumuisha malazi, milo, usafiri kwa magari maalum ya safari, viingilio katika hifadhi pamoja na huduma za
waongoza wageni wenye uzoefu.
Kupitia kampeni
hizi, Zara Tanzania
Adventures imeendelea kusisitiza umuhimu wa Watanzania kuwa sehemu ya utalii wa nchi yao badala ya kuishia kusikia
au kuona vivutio hivyo kupitia
wageni kutoka mataifa mengine.
Taasisi za Serikali, kampuni
binafsi, mashirika, vikundi
vya kijamii, vyuo na makundi mbalimbali yamehamasishwa kuunda timu
na kushiriki katika
Twenzetu Kileleni na Twenzetu Serengeti kama mojawapo ya njia za kuonyesha,
kuhamasisha na kudumisha
uzalendo, kuimarisha mshikamano
na kuongeza uelewa kuhusu
thamani ya rasilimali za utalii zilizopo nchini.
Ujumbe mkuu wa kampeni hizo ni kuwahamasisha
Watanzania kutembelea, kuthamini na
kujivunia urithi wao wenyewe.
Desemba
hii, tusibaki kusikia habari za Kilimanjaro na Serengeti — twende wenyewe.
Twenzetu Kileleni –
Msimu wa 5. Twenzetu Serengeti. Safari ni yetu, Mlima ni wetu, Serengeti ni yetu, Tanzania ni yetu.
Comments
Post a Comment