Clean Up Day - Moshi Kilimanjaro
Kampuni ya utalii Zara Tours imeshiriki zoezi la Kufanya usafi mkoani Kilimanjaro, ukiwa ni mwendelezo wa mkakati wake wa pamoja na taasisi ya Mount Kilimanjaro Porters Society MKPS, TESO, Zara Charity Tanzania Pamoja na Mkuu Wa Mkoa Wa Kilimanjaro na wadau wengine, kufanya usafi mkoani Kilimanjaro, katika kuadhimisha Wiki ya Usafi Duniani 2018. Zoezi la usafi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya usafi Duniani limeongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mheshimiwa Anna Mghwira Ambae alisema kuwa jukumu la usafi wa mazingira ni la kila mmoja na kupongeza kampuni ya Zara Tours na wadau wake kwa jitihada wanazofanya kulipa kipaumbele suala la kutunza mazingira.
Comments
Post a Comment